BREAKING: TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZAA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE

Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV,
AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa  kwa
huduma hizo zitapokuwa tayari.
Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James
Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa
sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
“Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and
postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma
zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano”,
imesema barua hiyo.
Wamiliki wa mitandao hiyo – Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi
na Abdallah Mrisho –  wameeleza
kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.
              
“Gloval
TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili – kama zingekuwepo – na
kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati
tunasubiria kanuni hizo mpya,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa
Global Publishers.
Ankal Michuzi na Millard  Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja
watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi
ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa. 
Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa
kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.
“Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii”, alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.
Ayo TV, Michuzi TV na Global TV,  ambazo zinaongoza kwa mbali kwa kutazamwa na
watu wengi nchini na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa
TCRA, kati ya vituo mtandao  takriban 51
vilivyopata barua hiyo.
Ankal Issa Michuzi wa Michuzi TV, Millard Ayo na Askofu wa Ayo TV na Abdallah Mrisho wa Global TV wakitoka makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano walikoitwa kuchukua barua zao zinazowazuia kuendelea kutoa huduma za TV mtandao hadi hapo kanuni za usajili na leseni utapokamilika.

from Blogger http://ift.tt/2lsG87X
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment