Tarehe 26
Feburari jua litapatwa kipete. Hali hii inatokea wakati umbali kati ya
mwezi na dunia unapokuwa mbali zaidi na umbali kati ya jua na dunia
unapokuwa karibu kuliko siku za kawaida, mwezi utaonekana kuwa mdogo
zaidi na hauwezi kufunika jua kikamilifu. Hali hii itaanzia nchini Chile
na Argentina katika bara la Amerika Kusini, kupita bahari ya Atlantiki,
na kuishia kusini magharibi mwa Afrika.
Tarehe 11 Agosti
jua litapatwa kikamilifu. Hali hii inaanzia kaskazini mashariki mwa
bahari ya Pasifiki, kupita Marekani na kuishia katika bahari ya
Atlantiki.
Mjumbe wa
shirika la unajimu la China Bw. Shi Zhicheng alifahamisha kuwa, mtu
akikaa katika sehemu moja tu, kwa wastani anahitaji kusubiri miaka 400
hivi kuona hali ya kupatwa kikamilifu kwa jua, hivyo watu wenye hamu ya
kutazama tukio hili wanaweza kutazama kupitia mtandao wa Internet au
kwenda nchi nyingine.
Hali ya kupatwa
kwa mwezi pia inastahili kutazama. Tarehe 11 Februari mwezi utaingia
mahali penye kivuli kidogo tu (partial shadow) cha dunia, hivyo kwa watu
wa kawaida, hawatagundua mwezi kupatwa, wataona tu mwanga wa mwezi
umepungua kidogo. Tarehe 8 Agosti mwezi utapatwa kisehemu, hali hii
itaonekana katika sehemu nyingi duniani ikiwemo Afrika.
0 maoni:
Post a Comment