Wabunge wa upinzani nchini Afrika Kusini waliokuwa wamevalia nguo nyekundu wakiongozwa na Mbunge machachari, Bw. Julius Malema jana walisimama Bungeni wakigomea ruhusa aliyopewa Rais Jacob Zuma kulihutubia Bunge la nchi hiyo.
Pamoja na kutakiwa kukaa kwenye viti vyao au kutoka nje kwa amani, wabunge hao waligoma kufanya kila waliloamrishwa na Spika wa Bunge hilo, Bi. Baleka Mbete na ndipo askari wa Bunge walipoamua kuwatoa wabunge hao kutoka ukumbini humo.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mmusi Maimane akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutolewa amesema kuwa kitendo hicho cha kutumia mabavu ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo na kuwataka askari kufuata sheria za nchi kwani wao wanafanya kazi kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi hiyo.
Mmusi Maimane, kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani katika Bunge la Afrika Kusini
Tazama hapa video ya tafrani hilo:
from Blogger http://ift.tt/2lrD3J4
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment