Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amekemea
tabia ya ukamatwaji wa wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge na
kusema kuwa jambo hilo ni kinyume cha sheria na utaratibu.
Akihitimisha
mkutano wa sita wa Bunge, Ndugai amesema kama kuna kiongozi yeyote wa
serikali anamuhitaji mbunge, anapaswa kutoa taarifa kwake kwanza badala
ya kwenda "kibabe".
Pia
Ndugai amewatoa hofu wabunge kuhusu hadhi ya Bunge na kusema kuwa hadhi
ya chombo hicho haijashuka, na kwamba Muhimili huo wa Bunge hauna
mgogoro wowote na serikali wala mahakama.
Pia
ameeleza madhara ya kukosekana kwa mbunge hata mmoja akisema kuwa yeye
kama Spika anapoitisha kikao cha kamati fulani, ni lazima akidi itimie,
vinginevyo kukosekana kwa mbunge hata mmoja kuna athari kubwa katika
maamuzi ya kikao na Bunge kwa ujumla.
Hatua
hiyo inafuatia malalamiko ya wabunge wa upinzani yaliyotolewa hivi
karibuni juu ya utaratibu unaotumiwa na Jeshi la Polisi kukamata wabunge
wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge, wakitolea mfano wabunge Tundu Lissu
na Godbless Lema.
Malalamiko
hayo yalifikia hatua ya mbunge Zitto Kabwe kutoa hoja akitaka kiti cha
Spika kitoe maamuzi ya kulinda hadhi ya Bunge kutokana na kukamatwa kwa
Tundu Lissu, hoja ambayo Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson aliipangua, jambo
lililopelekea wabunge wote wa upinzani wasusie kikao cha Bunge cha
jioni ya Februari 8, 2017.
0 maoni:
Post a Comment