ZIJUE ISHARA 5 KWAMBA UTAKUWA MILIONEA

Dola milioni moja za kimarekani kwa sasa haina thamani kubwa kama ilivyokuwa miaka ya 1980. Kipindi hicho ilikuwa ni sawa na kusema kwa sasa kuitafuta dola milioni tatu (karibia bilioni 7 za Tanzania). Hata hivyo, kufikia kiwango cha kuitwa milionea si jambo dogo la kusema utafumba na kufumbua macho tu ujikute ushakuwa.
Unaingizwa kwenye kiwango hiki endapo kwanza una umri wa kati ya miaka 21 na 49 ukiwa na kipato cha mwaka cha walau shilingi milioni 220 kwa mwa na pia uwe na kati ya shilingi milioni 110 hadi shilingi milioni 558 ambazo umewekeza. Jarida la Fidelity limesema kuwa watu wanaotimiza vigezo hivi wana vitu vitano vinavyofanana na mamilionea wa kipindi hiki:
1. Shughuli zinazowapatia faida kubwa: Matajiri wanaoibuka sasa wanajihusisha sana na masuala ya teknolojia, fedha na uhasibu—kama walivyokuwa wakifanya mamilionea wengi wa sasa wakati wakiwa wanautafuta umilionea wao miaka ya nyuma.
2. Wana kipato kikubwa: kipato cha kawaida kabisa kwa watu wa aina hii ni shilingi milioni 280, zaidi ya mara tano ya kipato cha watu wa kawaida. Hii inamaanisha wana nafasi nzuri zaidi ya kuweka akiba na wapo kwenye nafasi ya kupata kipato kikubwa zaidi ya hapo.
3. Walianza shughuli zao wenyewe: watu nane kati ya kumi kati ya mamilionea wapya wanaoibuka sasa hivi wameweza kuwekeza kutokana na juhudi zao binafsi, au wameongeza kiasi kikubwa juu ya kile walichokirithi, kitu ambacho mamilionea na wengine wenye kipato zaidi ya hapo wamekifanya kwa miaka mingi.
4. Wana malengo ya mbali sana: Kati ya mamilionea wane wanaoibuka sasa, watatu huwa wanafanya shughuli zao kwa kuweka malengo ya mbali wakiwa wanawekeza pesa zao kwenye miradi mbalimbali. Wanakuwa kama watu ambao ni matajiri wa muda mrefu, kundi hili la watu nao hubaki na biashara zao walizozianzisha kwa nyakati zote za kupanda na kushuka kwa uchumi badala ya kujaribu kutafuta soko la kutengeneza faida ya haraka haraka.
5. Ujasiri unaohitajika: Kama walivyo matajiri kupindukia, mamilionea hawa wanaoibuka kipindi hiki pia wanaonesha ujasiri wao kwa kuwekeza kwenye vitega uchumi vinavyoweza kuhatarisha kupotea kwa pesa zao, lakini vikiwa na uwezo wa kurejesha faida kubwa sana baada ya muda mrefu.
Kuwa milionea kwa vijana wa karne hii si jambo gumu sana. Kinachotakiwa ni nidhamu katika fedha na kuanza shughuli zako mapema katika maisha yako.

from Blogger http://ift.tt/2kSwSgw
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment