WANANCHI WA KATA YA SARANGA KUPIGA KURA JUMAPILI


 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WANANCHI wa Kata ya Saranga Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kujitokeza kupiga kura ya Diwani Novemba 15 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa kufanya uchaguzi huo kunatokana na kuharibika kwa uchaguzi wa Oktoba 25 ulisababishwa na vurugu.

Amesema wananchi wanaotakiwa kupiga kura kwa kata hiyo ni wale waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Natty amesema waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura  ni 58,611 ambao ndio wataoruhusiwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa diwani wanayemtaka kuongoza kata hiyo.

Amesema vituo vya kupiga vitafunguliwa majira ya saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na baada ya hapo zoezi likiwa limekamilika la uhesabiaji kura atatangazwa mshindi katika uchaguzi huo.

Uchaguzi wa diwani katika kata hiyo ilitokana na vurugu kubwa ambazo zilianza majira ya 11:000 asubuhi ilifanywa na baadhi ya wasimamizi wa vituo na watu wasiojulikana katika cha kugawa vifaa eneo TANROAD Temboni.

from Blogger http://ift.tt/1Ps5Ju3
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment