Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amesema mnamo tarehe 14.8.2013 ajira ya saa 16;50 eneo la Airport Tankini kulifanyika unyang'anyi wa pikipiki aina ya T.691 CJF aina ya KINGLION uliofanywa na watu wawili.
![]() |
| moja ya pikipiki 8 www.jichopembuzi@gmail.com |
Aidha Diwani ameongezea kuwa aliye porwa pikipiki ni Daniel Songela mkazi wa Mbalizi alinyang'anywa na watu wa 2 waitwao Baraka Daudi,na Shadrack Essau na wote ni w
akazi wa jiji la Mbeya.
Hata hivyo sambamba na tukio hilo jumla ya pikipiki nane zinazo dhaniwa kuwa mali ya wizi zimekamatwa katika msako huko Tukuyu wilayani rungwe na watuhumiwa 6 wamekamatwa akiwemo Simon Mwanyasi,Lwitiko Hadson,Osfa Mwamakula,Festo Gideon,Sofia Gideon,Noel Yesaya na wote ni wakazi wa Tukuyu.Kamanda Athumani anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kupata mali kwa njia ya mkato kwa tamaa za utajili wa haraka kwani ni kinyume cha sheria.

0 maoni:
Post a Comment