Viongozi
nchini Guinea wamesema tayari wamepata maiti kadhaa za timu ya wahudumu
wa afya pamoja na wanahabari waliotoweka walipokuwa wakiendeleza
harakati za kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu ugonjwa wa
Ebola.
Msemaji wa serikali ya Guinea amesema kati ya miili hiyo ni ile ya wanahabari watatu wa timu hiyo.
Timu
hiyo ilisemekana kupotea baada ya kushambuliwa hapo jumanne katika
kijiji kimoja kilicho karibu na Mji wa Nzerekore ulio kusini mwa Guinea.
Mkurupuko
wa Ugonjwa huo ndio hatari zaidi kote duniani kwa sasa, huku viongozi
wakitahadharisha kwamba huenda watu zaidi ya 20,000 wakaambukizwa.
Timu
hiyo ya madaktari watatu na wanahabari watu walipotea baada ya
kushambuliwa kwa mawe na wakaazi wa kijiji cha Wome, walipofika katika
kijiji hicho kilicho karibu na mahala ambapo mkurupuko wa Ebola ulianza. Kwa mujibu wa mwanahabari mmoja
aliyeweza kunusurika aliwaambia wanaripota kwamba alipokuwa amejificha,
aliweza kusikia wakaazi hao wa Wome wakiwatafuta.
Wajumbe wa
serikali wakiongozwa na Waziri wa Afya walitumwa maeneo hayo lakini
hawangeweza kufika kwa kutumia barabara kwani daraja lilikuwa limewekwa
vizuizi.
Hapo Alhamisi msemaji wa serikali ya Guniea Albert
Damantang Camara alithibitisha kwamba maiti nane zilikuwa zimepatikana
na miongoni mwazo zilikuwa zile za wanahabari watatu.
Alieleza ya
kwamba miili hiyo ilipatikana katika pipa moja la shule ya msingi iliyo
katika kijiji hicho, na kuongeza kuwa timu hiyo iliuawa kinyama na
wakaazi hao.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment