Msikiti wa
Sogea uliopo jirani na Branchi ya Sogea unawaomba Waislamu popote mlipo
katika ulimwengu huu wa Arrahmaan kuungana nao katika kukimaliza kisima
cha maji kilichopo nje ya Msikiti ambacho kilianzwa kuchimbwa kwa juhudi
za Waislamu ila wameishiwa nguvu na hivyo kuwaomba Waislamu Sadaka
zao.
Kisima imebidi
kiongezwe chengine baada ya kuzidiwa nguvu kwa kisima kilichopo sasa
ambacho hakitoshelezi mahitaji ya maji kwa msikiti kutokana na wingi wa
Waislamu wanaokufika msikitini kwa shughuli za Ibada.
Gharama iliyobakia kumalizia kisima hiki ni takriban Shilingi Milioni moja na Nusu tu.
Ndugu yangu
Muislamu na katika Imani, jitahidi isikupite fursa hii adhimu na adimu
ya kujiwekea akiba isiyooza au kuharibika huko tuendako kwa kutoa
Sadaqatun Jaariyah (Sadaka yenye kuendelea)
Allaah
Subhaanahu Wata'ala anatukumbusha katika Qur'aan "Na kheri yoyote
mtakayoitanguliza kwa ajili yenu basi mtaikuta mbele ya Allaah itakuwa
kheri kubwa na (yenye) ujira mkubwa" Suuratul Muzammil
Kwa maelezo zaidi na vipi kuwasilisha sadaka yako, wasiliana na Imaam wa Msikiti wa Sogea Sheikh Suleiman Bin Daaud +255 777 460 056
Sehemu ya eneo
la kisima ambacho mbali na kutoa maji na kuhudumia Msikiti pia wakaazi
wanaoishi maeneo ya karibu hutegemea kisima cha msikiti kwa kupata
huduma hii iliyoadimika ya maji kwa kuchangia msikiti.
Msikiti wa Sogea ambao upo Barabarani na waumini wengi hufika kwa kusali Sala tano pamoja na Sala ya Ijumaa. Msikiti huwa unajaa wakati mwengine mpaka watu kukosa kusali
Sehemu ya kisima chenyewe ambacho kimefunikwa kwa sasa ili kisiharibike
0 maoni:
Post a Comment