Denti ,Alpha Mohamed (18) anayedaiwa kupigwa na Diwani wa Kata ya Sinza kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Renatus Pamba, ‘Mr Simple’.
Mwanafunzi
wa Chuo cha Ubaharia (EMI) kilichopo Posta jijini Dar, Alpha Mohamed
(18) aliyedaiwa kupigwa na Diwani wa Kata ya Sinza kwa ‘leseni’ ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Renatus Pamba, ‘Mr Simple’, bado
yu hoi katika Hospitali ya Mwananyamala, DarAlpha alidaiwa
kupigwa Agosti 29, mwaka huu nyumbani kwa diwani huyo Sinza- White Inn,
Dar ambapo chanzo cha kipigo hicho kilisemekana kuwa ni denti huyo
kukutwa akipiga stori na binti wa diwani aliyejulikana kwa jina moja la
Mage.
Ilidaiwa
kwamba baada ya vipimo ilibainika kwamba denti huyo alipata maumivu
makali kifuani na mgongoni baada ya kupigwa na fimbo pamoja na fagio.
Chanzo
chetu kilibaini licha ya Alpha kupelekwa katika Hospitali ya Palestina
iliyopo Sinza jijini Dar lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwani mara kwa
mara amekuwa akitapika damu na kulalamika kupata maumivu makali maeneo
ya kifua na kichwani huku akikohoa damu.
Ilisemekana
kwamba kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya, ndugu wa Alpha wamelazimika
kupitisha karatasi ya michango mtaa mzima kumchangia fedha za matibabu
ili kunusuru maisha yake.
Alipotafutwa mjomba wa Alpha, Aboubakari Ramadhani ili kujua afya ya Alpha, alisema bado haijatengemaa na amelazwa Mwananyamala.
Alipotafutwa mjomba wa Alpha, Aboubakari Ramadhani ili kujua afya ya Alpha, alisema bado haijatengemaa na amelazwa Mwananyamala.
“Hali
yake ni mbaya, hatujui nini kitatokea. Familia ilifungua jalada la kesi
lenye kumbukumbu KN/RB/7748/2014 SHAMBULIO hivyo tunaendelea kumtibu
huku tukisubiri hatua za kisheria,” alisema Ramadhani.Baada ya habari ya
tukio hilo kuripotiwa kwenye gazeti hili toleo Na 1145 lenye kichwa cha
habari kilichosomeka;
DIWANI
AMPA KIPIGO DENTI, wanahabari wetu walimtafuta diwani huyo ili kujua
undani wa sakata hilo kwani naye alifungua mashitaka akidai Alpha
alimbaka bintiye, lakini hakutoa ushirikiano.
Kwa nyakati tofauti, sakata hilo limeripotiwa katika vituo viwili tofauti vya polisi, Kijitonyama-Mabatini alikoshitakiwa diwani na Urafiki-Ubungo ambako diwani alimshitaki Alpha akidai alimbaka bintiye, Mage.
Kwa nyakati tofauti, sakata hilo limeripotiwa katika vituo viwili tofauti vya polisi, Kijitonyama-Mabatini alikoshitakiwa diwani na Urafiki-Ubungo ambako diwani alimshitaki Alpha akidai alimbaka bintiye, Mage.
0 maoni:
Post a Comment