Rais wa
Marekani Barrack Obama hii leo anatazamiwa kutangaza mpango wake wa
kuwatuma wanajeshi 3,000 nchini Liberia kama njia moja ya kusaidia
katika vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Wanajeshi hao
watasimamia ujenzi wa vituo vipya vya kimatibabu na pia watahusika
katika utoaji wa mafunzo ya kimatibabu kwa wahudumu.
Kumekuwa na
malalamishi kwamba jamii ya kimataifa imelegea katika harakati za
kukabiliana na mkurupuko wa Ebole katika mataifa ya Afrika magharibi. Wanajeshi hao watatumika kuunda muundo msingi wa kupamabana na Ebola Liberia
Mataifa ya Sierra Leone,
Liberia na Guinea ndiyo yaliyoathirika zaidi huku zaidi ya watu 2,400
wakiwa tayari wamepoteza maisha yao kufikia sasa.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huu ni raia wa Liberia.
Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha kuwa huenda watu zaidi wakazidi kufariki.
Umoja
wa Mataifa (UN) unapangiwa kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na mlipuko
wa ugonjwa wa Ebola katika mkutano unaopangiwa kufanyika huko Geneva.
Kulingana na viongozi nchini Marekani, mpango wao wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unalenga-: Zaidi watu 2400 wameaga dunia kutokana na Ebola
Utoaji wa mafunzo ya kimatibabu kwa wahudumu wa kiafya 500 kila juma.
Ujenzi wa vituo vya matibabu 17, kila chumba kikiwa na vitanda kumi.
Usambazaji
wa vifaa vya huduma ya afya kwa kila nyumbaKampeni ya kuwahamasisha
wananchi kuhusu jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa wa Ebola.
Ujenzi
wa kituo cha kijeshi cha pamoja mjini Monrovia kitakachotumiwa katika
shughuli ya kupokea msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Wadadisi
wa masuala ya kimatibabu wamepongeza mpango huu wa Marekani huku
wengine wakitilia shaka nia ya Marekani nchini Liberia.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment