UTAFITI
uliofanywa na mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia
uwezekano wa vijana kupunguza ngono, umebainisha elimu ya afya ya uzazi
bado inahitajika ili kuwakinga na tabia hatarishi.
Akitoa
matokeo ya awali ya utafiti huo, mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili, kitengo cha magonjwa na afya
ya akili, Lusajo Kajula, alisema kuwa asilimia 10 ya vijana wenye umri
wa miaka 12 hadi 14 ambao ni wanafunzi wa darasa la tano na sita
wameshawahi kufanya ngono.
Alisema ngono hiyo kwa asilimia kubwa hufanywa na wanafunzi hao kinyume na maumbile.
Kajula alisema vijana wengi wamebainika kufanya ngono ya kawaida na ya mdomo, ikifuatiwa na ngono ya kinyume na maumbile.
Alisema
kwa wale ambao wameshawahi kufanya ngono, asilimia 6.3 wamefanya
kinyume na maumbile wakati asilimia 93.7 hawajawahi kufanya.
Alisema utumiaji wa kondomu umebainika kuwa mdogo kwa vijana wadogo ambao wameanza kufanya ngono.
“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajawahi kutumia kondomu kabisa, wakati asilimia 32 wamewahi kutumia,” alisema.
Alisema
hiyo ni sehemu ya utafiti wa miaka minne ulioshirikisha Chuo Kikuu cha
Makerere cha Uganda, Cape Town na Limpopo vya Afrika Kusini, Bergen na
Oslo vya Norway, Maastricht cha Uholanzi na Sussex cha Uingereza.
Katika
utekelezaji wa utafiti huo, wanafunzi 5,099 walichaguliwa mwanzoni mwa
mradi kufanyiwa utafiti huo, ambapo 4,783 (asilimia 93.9)
walifuatiliwa kwa miezi 6 na wengine 4,370 (asilimia 85.8) kwa miezi
12.
Mradi
huo wa PREPARE ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka Manispaa ya
Kinondoni zilizochaguliwa, kwa kutumia sampuli mtawanyiko, zilizopangwa
katika makundi mawili ya shule.
“Kimsingi
tunataka kuwaambia wanahabari kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya
mradi wa PREPARE ni kuchelewesha kuanza ngono miongoni mwa wanafunzi wa
kiume na wa kike wenye umri wa miaka 12-14 katika Mkoa wa Dar es
Salaam,” alisema Kajula.
Matokeo
yaliyotathminiwa ni mabadiliko katika masuala ya ngono (kuanza ngono)
na kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa wale waliokwishaanza
vitendo hivyo.
Kajula
alisema kwa wastani mradi wa PREPARE umefanikiwa kupunguza uwezekano
wa vijana wadogo hasa wavulana na wasichana kuanza ngono na kuongeza
matumizi ya kondomu kwa wale walioanza.
Hata
hivyo, katika utekelezaji wa mradi mabadiliko katika uchukuaji wa
hatua yalionekana zaidi miongoni mwa wasichana waliopata mwingilio
ukilinganisha na wale ambao hawakupata.
Alisema
uchukuaji wa hatua ulisababisha kuwapo tabia ya kutumia kondomu kwa
wanafunzi wa jinsia zote na taarifa za ongezeko la utumiaji wa kondomu
miongoni mwa vijana wa kiume.
Kajula alisema ili kuweza kupata matokeo yaliyokusudiwa, mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watano wakufunzi wa wakufunzi.
Alisema
mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watekelezaji 76, na waelimishaji rika
wanafunzi 132 na kuelekeza watoa huduma 8 wa afya katika kliniki za
huduma rafiki kwa vijana ili kutekeleza mwingiliano.
Mradi
huo umefadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya, ambapo programu ya utafiti
wa afya imelenga kuangalia mwingilio ulio katika misingi ya utamaduni
na jinsia, endelevu, kijamii ili kukuza ujinsia na afya ya uzazi
miongoni mwa vijana wenye umri miaka 12-14 kwa kutumia shule kama njia
ya kufundishia.
Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo, alisema utafiti umeonyesha haja ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wadogo ambao bado hawajaanza ngono ili kuchelewesha kuanza ngono kwa mfumo wa kisaikolojia kama njia ya kufanya wajitambue

0 maoni:
Post a Comment