WHO:Visa vya Ebola vimeongezeka kwa kasi

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya visa vipya vya ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika inaongezeka kwa kasi mno kwa mamlaka kuweza kuvidhibiti.
Shirika hilo linasema kuwa zaidi ya watu 2,400 wanadaiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo huku zaidi ya watu 4,800 wakidaiwa kuambukizwa.
Kwa mara nyengine shirika hilo limetoa wito kwa maafisa wa afya kote duniani kuelekea katika eneo hilo ili kutoa usaidizi.
Awali Cuba ilitangaza kuwa inawatuma zaidi ya maafisa 160 wa afya nchini Sierra Leone.
Waziri wa afya nchini Cuba Roberto Morales Ojeda amesema kuwa madaktari wa kwanza na wauguzi watawasili mapema mwezi ujao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment