
Tume ya Ulaya imeitaka Uhispania kueleza ambavyo muuguzi aliambukizwa
Ebola mjini Madrid na kumfanya kuwa mtu wa kwanza kuambukizwa ugonjwa
huo nchini humo kutoka Afrika Magharibi.
Muuguzi huyo ambaye amewekwa karantini alikuwa sehemu ya kukindi cha
matabibu waliowatibu wamishonari wawili waliofariki kutokana na ugonjwa
huo nchini humo.
Maafisa wa Afya nchini hispania wanasema kuwa muuguzi huyo anapokea matibabu.
Maafisa wakuu wanasema kuwa watu wnegine watatu wanachunguzwa
hospitalini baada ya kushukiwa kuwa na dalili za Ebola. Watatu hao ni
pamoja na mumewe muuguzi huyo , mfanyakazi mwingine wa afya na msafiri
mmoja kutoka Afrika Magharibi.
Afisa mmoja wa afya nchini Hispania anasema kuwa muuguzi huyo angetengwa awali baada ya kugundulika kuwa na virusi hivyo.
Takriban watu 3,400 wamefariki kutokana na Ebola wengi wao wakiwa Afrika Magharibi.
Muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 40,ambaye hajatajwa alikuwa anafanya
kazi katika hospitali ya Carlos 111 mjini Madrid na alihusika katika
juhudi za kuwatibu makasisi Maneul Garcia na Miguel Pajares waliofariki
kutokana na Ebola.
Wote waliambukizwa Ebola wakiwa nchini Liberia katika shughuli za kimishionari.
Muuguzi huyo aliingia katika chumba alimokuwa mmoja wa wamishionari hao
kumhuduumia na kusaficha chumba hicho baada ya kifo cha mmoja wao. Hata
hivyo nyakati zote alipokuwa anafnya kazi yake alikuwa amevalia magwanda
ya kujikinga kutokana na maambukizi
Maafisa wa afya wanasema hawajui chanzo cha maambukizi kwa muuguzi huyo
maana alikuwa amevalia magwanda na hapoakuwa na taarifa za ajali yoyote
iliyomuweka muuguzi huyo katika hatari ya kuambukizwa.
0 maoni:
Post a Comment