JAMII Mkoani Njombe,
imeombwa kujitokeza kuwaasili (Kuwa chukua kama ndugu) watoto yatima
wanaolelewa katika vituo vya yatima, ambao wazazi wao wamefariki ama watoto hao
waliookototwa baada ya kutelekezwa muda mfupi baada ya kuzaliwa
ambao wazazi hawatambuliki.
Wito huo umetolewa na
Katika kituo cha yatima ilichopo Hospitali Teule ya Ilembula ,
inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya
Kusini wakati akipokea misaada kutoka Benki ya CRDB Tawi la Makambako.
Kituo hicho chenye
watoto 12, kati yake wawili wakiwa hawajulikani wazazi wao baada ya kuokotwa
wakiwa wametelekezwa muda mfupi bada ya kuzaliwa, na kuhudumiwa na hospitali
hiyo kupitia mradi shirikishi
kati ya serikali na Taasisi binafsi (PPP).
Akipokea msaada huo wenye
thamani ya sh. Milioni 1.1, Katibu Utawala wa Hospitali hiyo Bryceson
Mbilinyi alisema, kituo kina changamoto ya walezi au ndugu kushindwa kuchangia fedha kiasi
sh. 2000 tu kila mwezi pamoja na kuwatelekeza watoto kituoni.
Msaada huo umepokelewa
kwa shangwe kituoni hapo, na kwamba utapunguza adha zinazowakabili, lakini pia
Wito ukatolewa kwa wadau wengine.
Meneja wa CRDB Tawi la
Makambako, Denis Moleka akiongoza timu ya wafanyakazi alisema, ziara ya
kutembelea kituo hicho ni sehemu ya wiki la huduma kwa wateja ambayo hufanyika
kila mwaka, ambapo Benki hiyo hurudisha fadhira kwa wananchi.
“Benki ya CRDB inampango
wake wa kurudisha fadhira kwa wananchi jamii kwa ujumla,asilimia 1 ya faida
yake kila mwaka hutumika kwaajili ya kutoa misaada kwa wahitaji hilo ni kwa
makao makuu na matawini kwa ujumla”Alisema Moleka.
Upande wao wafanyakazi
wa CRDB wakaguswa sana na taarifa ya watoto waliopo kituoni hapo Flora Fuime
alisema, ziara hiyo imempa somo kubwa katika maisha yake na kutambua umuhimu wa
kujenga tabia ya kuwatembelea mazingira ya wahitaji.
Akizungumzia kuhusu
wazazi wanaowatupa watoto baada ya kuzaliwa,Peter Mwambembe ofisa wa Benki alisema, uzazi wa
mpango inahitajika katika jamii ili kuepusha vifo vya mama wajawazito na watoto
wachanga.
“Mimi nadhani suala la
yatima haliepukiki lakini kama tutajikita katika kupanga uzazi vifo vya akina mama
vitapungua na kuwa na idadi ndogo ya yatima kama hawa, nawashauri wazazi
wenzangu kuzingatia sana uzazi wa mpango”Alisema, Mwambembe.
0 maoni:
Post a Comment