Waendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC
wamewaomba majaji wa mahakama hiyo waamue kwamba Kenya
haitoi ushirikiano katika kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu
inayomkabili rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta. Mwendesha
mashtaka wa ngazi ya juu wa mahakama hiyo Ben Gumpert
ameliambia jopo la majaji watatu leo Kenya haitawasilisha vitu
wanavyotaka na vilivyoidhinishwa na mahakama hiyo kwamba
wanaweza kuviitisha kama ushahidi kutoka kwa nchi hiyo. Iwapo
majaji watapitisha uamuzi huo suala hilo litawasilishwa kwa baraza la
nchi wanachama, ambalo ni chombo kinachoziwakilisha nchi
zilizosaini mkataba wa Roma uliotumiwa kuiunda mahakama ya ICC.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment