Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika
eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana
na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji.
Katibu Mkuu wa Chama
cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi
tatizo la wakulima wa chai katika Jimbo la Bumbuli ndani ya mwezi mmoja
ujao. Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara
katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa
kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji. Kinana aliwalaumu
viongozi wa Serikali ya mkoa kutumia muda mrefu kushughulikia matatizo
ya wakulima na kutolea mfano tatizo la kiwanda hicho lililoanza mwaka
2008. “Mgogoro huu ni wa siku nyingi, watu wanatupiana mpira
tu...Badala ya kuchukua hatua kuutatua, wao wanaleta porojo. Viongozi wa
Serikali wanawapuuza wakulima wakati wao mambo yao yako safi,”
alisema. Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa atalifikisha suala hilo
katika Kamati Kuu ya CCM inayohudhuriwa na viongozi wote wa juu nchini.
“Tutakwenda kujifungia na kuulizana maswali magumu... ni lazima
walioshindwa kulishughulikia suala hili wawajibike, kama hawataki
kuwajibika kwa hiari basi wawajibishwe,” alisema. Alibainisha kuwa
kumekuwa na kulindana ndani ya Serikali na ndio maana viongozi
wanaoshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi wanaendelea na utumishi
bila ya kuchukuliwa hatua zozote kwa haraka. Awali, wananchi
waliohudhuria mkutano huo walimtimua diwani wao, Richard Mbuguni ambaye
walimtuhumu kushirikiana na mwekezaji huyo kuwadhulumu wakulima.
Wananchi hao walifanya hivyo baada ya mwenyekiti wa wakulima wadogo wa
chai katika eneo hilo, Almas Shamshama kumtaka kiongozi huyo kuondoka
katika mkutano huo.Kinana aahidi kusaidia wakulima Mponde SHARE
BOOKMARKPRINTEMAILRATING Na Rais Said, Mwananchi Posted
Jumatano,Oktoba1 2014 saa 8:14 AM KWA UFUPI Alitoa ahadi hiyo juzi
jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na
kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima
na mwekezaji. SHARE THIS STORY 0 inShare Bumbuli. Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameahidi kulitafutia
ufumbuzi tatizo la wakulima wa chai katika Jimbo la Bumbuli ndani ya
mwezi mmoja ujao. Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa
hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho
kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji. Kinana
aliwalaumu viongozi wa Serikali ya mkoa kutumia muda mrefu kushughulikia
matatizo ya wakulima na kutolea mfano tatizo la kiwanda hicho
lililoanza mwaka 2008. “Mgogoro huu ni wa siku nyingi, watu wanatupiana
mpira tu...Badala ya kuchukua hatua kuutatua, wao wanaleta porojo.
Viongozi wa Serikali wanawapuuza wakulima wakati wao mambo yao yako
safi,” alisema. Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa atalifikisha suala
hilo katika Kamati Kuu ya CCM inayohudhuriwa na viongozi wote wa juu
nchini. “Tutakwenda kujifungia na kuulizana maswali magumu... ni lazima
walioshindwa kulishughulikia suala hili wawajibike, kama hawataki
kuwajibika kwa hiari basi wawajibishwe,” alisema. Alibainisha kuwa
kumekuwa na kulindana ndani ya Serikali na ndio maana viongozi
wanaoshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi wanaendelea na utumishi
bila ya kuchukuliwa hatua zozote kwa haraka. Awali, wananchi
waliohudhuria mkutano huo walimtimua diwani wao, Richard Mbuguni ambaye
walimtuhumu kushirikiana na mwekezaji huyo kuwadhulumu wakulima.
Wananchi hao walifanya hivyo baada ya mwenyekiti wa wakulima wadogo wa
chai katika eneo hilo, Almas Shamshama kumtaka kiongozi huyo kuondoka
katika mkutano huo.
Na Mwananchi
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment