Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza na wananachi na wanavikundi vya ushirika katika kijiji cha Mvuleni Kidoti kutekeleza ahadi aliyowapa hivi karibuni ya kusaidia vikundi vya akina mama.
Mama Asha akimkabidhi fedha taslim shilingi 400,000/- Bibi Patima Jaku Ali wa Kikundi cha Ushirika cha Mola tubariki kinachojishughulisha na miradi ya dagaa.
Mama Asha akimkabidhi vyarahani Marobota na vifaa vyake Bibi Mboja Silima Juma wa Kikundi cha ushirika cha Hatuyumbishwi vitakavyowasaidia katika kazi zao.
Bibi Zubeda Silima Ali wa Kikundi cha Ushirika cha Chumvi Mvuleni katika kijiji cha Kidoti akifarjika b aada ya kupokea msaada wa Doti 50 za Kanga na Charahani kutoka kwa Mama Asha Suleiman Iddi aliyefika Kijijini hapo kutekeleza ahadi aliyowapa hivi karibuni




0 maoni:
Post a Comment