Maafisa wa India wamesema mamia ya watu wameyakimbia makazi
yao katika eneo la Kashmir huku wanajeshi wa nchi hiyo
wakikabiliana na vikosi vya Pakistan kwenye mapigano makali
ambayo mpaka sasa yamewaua watu tisa. Makabiliano ya risasi
katika eneo la mpakani ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika
siku za hivi karibuni yameibua wasiwasi mkubwa na watu tisa
waliuwawa jana pekee, idadi ya vifo inayoelezwa kuwa kubwa kwa
siku moja katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja katika eneo hilo.
Raia wapatao 10 wa India wamejeruhiwa wakati wanajeshi wa India
na Pakistan walipofyetuliana risasi katika eneo linalozozaniwa la
Kashmir kwa siku ya pili leo. India na Pakistan zimelaumiana kwa
kuchochea ufyetulianaji huo wa risasi ulioanza Jumapili iliyopita.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment