Mazrui hatimaye azikwa


Ali Mazrui
Msomi maarufu marehemu Profesa Ali Mazrui hatimaye amezikwa.
Mazrui alizikwa nyumbani kwao katika eneo la Old Town mjini Mombasa nchini Kenya.
Mwili wake uliwasili mapema jumapili kutoka nchini Marekani ambako amekuwa akiishi.
Msomi huyo alikuwa na tajriba kuu katika taaluma yake.
Mbali na kuwa mwalimu alisomea katika vyuo vikuu ikiwemo Oxford ambapo alijapatia shahada ya philosophia mwaka 1966.
Baadaye Mazrui alijiunga na Chuo kikuu cha Makerere kama mkuu wa kitengo cha sayansi ya siasa.
Vilevile ameweza kuandika vitabu chungu nzima ambavyo vitaendelea kuwa kumbukumbuku yake
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment