Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA)Ndg, Mbwana J.Mbwana akifungua Mkutano wa Umoja wa Vyuo vya
Usafiri wa Anga Barani Afrika, akihutubia wakati wa ufunguzi huo wa
mkutano wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya
Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika Ndg. Tchagbele
Sadamba, akizungumza na kutowa maelezo ya Umoja huo wakati wa Ufunguzi
wa Mkutasno wa Kwanza uliotayarishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani
Zanzibar.
Afisa wa Civil Avation Training Centre Bi Margareth Kyarwenda
akizungumza katika mkutano huo kuhusiana na mafunzo yanayotolewa na
Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika, wakati wa ufunguzi wa mkutano
huo uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar
na kushiriki Nchi wanachama wa Umoja huo barani Afrika.
Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga
Barani Afrika wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, akifungua
mkutano huo Zanzibar.
0 maoni:
Post a Comment