Mkuu wa Hong Kong awapuuza waandamanaji


Mmoja ya waandamanaji katika jimbo la Hong Kong
Mkuu wa eneo la Hong Kong amepuuza wito wa waandamanaji kuwa ajiuzulu na badala yake ametoa wito kwa wakaazi wa eneo hilo wakubali mabadiliko ya kisiasa yaliyopendekezwa na Serikali Kuu ya Uchina.
Sheria hizo zilizotangazwa mwisho wa Agosti, zimezusha maandamano ya maelfu ya watu katika eneo hilo lililokuwa wakati mmoja koloni ya Uingereza.
Akizungumza katika sherehe ya kitaifa ya Uchina, Mkuu wa Hong Kong, CY Leung, alisema kuwa kila mtu atakuwa na fursa ya kumpigia kura kiongozi katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanywa baada ya miaka mitatu, iwapo jiji hilo la Hong Kong litakubali kuidhinisha mabadiliko ya uchaguzi kama ilivyopendekezwa na Serikali Kuu ya Uchina.
Lakini maafisa wa Uchina wamesema kuwa ni wagombeaji ambao wanawaamini pekee ndio watakaopata fursa ya kuwania viti mwaka wa 2017.
Wazo hilo limekataliwa na makumi ya maelfu ya waandamanaji ambao sasa wamekalia barabara zote za Hong Kong wakitaka mamlaka kuamua ni nani anayestahili kugombea viti katika uchaguzi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment