Rais Sata asafiri nje kwa matibabu


Rais Sata anasemekana kuwa katika hali mbaya ya kiafya
Taarifa kutoka nchini Zambia zinasema kuwa Rais wa nchi hiyo,Michael Sata amesafiri nje ya nchi kwa matibabu kufuatia taarifa kuwa afya sio nzuri.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya Bwana Sata mwenye umri wa miaka 77 ilisema Rais amekwenda nje kwa matibabu ingawa haikusema ni katika nchi gani.
Rais Sata alijitokeza hadharani tarehe 19 Septemba kuambia bunge la taifa kuwa bado yuko hai.''Mimi sijafa'' alinukuliwa akisema Sata.
"Anajulikana kama ''King Cobra" kwa kauli zake kali, na alichaguliwa Raia wa Zambia mwaka 2011.
Haijabainika ikiwa atarejea Ijumaa kuongoza sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.
Bwana Sata hajaonekana hadharani tangu kurejea kutoka katika mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa mwezi jana ambako alikosa kutoa hutuba aliyotarajiwa kutoa.
Waziri wa ulinzi , Edgar Lungu, ameteuliwa kama Rais wa muda kufuatia hali mbaya ya afya inayokabili Rais Michael Sata
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment