Miss
Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa
habari. video ya alichokisema Miss Tanzania itawajia muda si mrefu.

Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa
mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea
na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali
wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu
(kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri
wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa
mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala
ya cheti cha kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wakazazi
wake.
Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991.
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
“Ukweli
ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho hapo kinajielezea, mkitaka
mnaweza kwenda hizo sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema Sitti.
Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha kuzaliwa kilipotea akidai
kuwa ni kutokana na maisha yake ya kusafiri mara kwa mara.
“Kwahiyo ilibidi pale walipohitaji cheti nilete kingine,” alijitetea.
“Sikutegemea
hayo maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo,” alijibu mrembo
huyo baada ya waandishi wa habari kumtaka awape ripoti yoyote ya polisi
kuhusiana na kupotea kwa cheti chake cha mwanzo.
Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.
Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,” alisema.
Akijibu
swali la kuonekana kwa passport yake inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka
1989 na huku kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa May 31,
1991, Sitti alisema:
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
Sitogusia
hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’
niliombwa cheti cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal life,
kwahiyo sidhani hata
nyie kama kuna mtu atakuja anachukua passport yetu, ama driving
licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye mtandao kama ni kitu ambacho
mngependelea.”
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited Hashim
Lundenga alisema kuwa nafasi ipo wazi kwa wale wenye mashaka na umri na
maisha ya Sitti kupeleka vielelezo halisi ambavyo watavifanyia kazi.
“Tukishapata proof tutazifanyia kazi vizuri sana na mwenye haki atapata. Sisi hatuwezi kumvua taji, vitahusika BASATA na wizara husika,” alisema Lundenga.
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
Kuhusu
Sitti kudanganya kuwa na umri wa miaka 18 kama watu walivyodai ndivyo
alivyosema, Lundega alidai kuwa hayo yamezushwa mtandaoni na kwenye
shindano hilo hakuna aliyesema hivyo.
“Unaamini
kwamba Sitti ana miaka 18?” alihoji Lundenga. “Sasa kama huamini yote
yametoka kwenye vyombo vya habari. Sisi tunaamini cheti cha kuzaliwa,
sasa kama kuna mtu ana doubt na cheti cha kuzaliwa aende RITA akafanye
uchunguzi wake.”
0 maoni:
Post a Comment