JESHI
la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamshikilia mchimba dhahabu, Shija Salum
(38), mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua rafiki yake
na kula ubongo wake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi wa
habari jana kwamba pamoja na mtuhumiwa huyo kula ubongo wa rafiki yake
huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Shija, pia alitafuna sehemu zake za
siri baada ya kuzikata.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari, tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka
huu, usiku katika Kijiji cha Manyanya, Kata ya Makongorosi, Wilaya ya
Chunya mkoani Mbeya.
Alisema mtuhumiwa na marehemu walifika kijijini hapo wakitokea Shinyanga miezi mitatu iliyopita.
“Inasemekana
wawili hao walikuwa ni marafiki kwani walifika wilayani Chunya, Kata ya
Makongolosi kwenye machimbo ya dhahabu yanayomilikiwa na mfanyabiashara
mmoja aitwaye Teddy Mwantega.
“Siku
hiyo ya tukio, marehemu Shija, alikuwa amejilaza mahali na hapo ndipo
alipofika rafiki yake huyo, akiwa na panga mkononi na kumkata kwa nguvu
kichwani.
“Baada ya hapo, alimvua nguo na kuzikata sehemu zake za siri na kuzishika mkononi.
“Wakati akiwa na sehemu hizo za siri mkononi, alichukua ubongo wa marehemu na kuula, kisha akatafuna zile sehemu za siri.
“Kwahiyo, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” alisema Kamanda Kidavashari.
0 maoni:
Post a Comment