Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Ritha Komba amesema kuwa wimbo huu wa Happy Birthday ni zawadi kwa watu wote ambao wanasherehekea kumbukumbu ya siku zao za kuzaliwa ikiwa ni sehemu ya kumshukuru Mungu kwa kwa neema ya uhai ambayo imewafanikisha kuwepo duniani hadi hivi leo.
“Watu kabla ya kusheherekea siku ya kuzaliwa wanatakiwa kutafakari ilikuaje wakati mama mzazi alipoenda leba na mpaka mtu anapata nafasi ya kusheherekea jua ni Mungu maana wakati Mtu huyo anazaliwa kuna mama alipoteza mtoto na mwingine alimuacha mtoto. Je watu wanashangilia tu siku ya kuzaliwa bila kutafakari? Au hawajui Siku hiyo ilikua ya namna gani? Mama apatapo uchungu pale hakuna furaha zaidi ya kuwa na hofu kwamba atajifungua salama? Je atatoka mzima yeye na mtoto? lakini anapozaliwa mtoto watu hufurahi na kumsifu Mungu na vivyo hivyo inapaswa watu wanaposherehekea kumbukumbu ya siku zao za kuzaliwa basi wanapaswa pia kupata Muda wa kutafakari na kumshukuru Mungu kwa neema ya uhai na afya inayomuwezesha kutenda yote kwa uwezo wa Mungu.”
Muimbaji Ritha Komba kwa sasa anatamba na album yake mpya inayoitwa Mungu wa Ajabu aliyoizindua hivi karibuni ikiwa kwenye mfumo wa Audio CD na DVD na kwa mara ya kwanza itaingia sokoni ndani ya mwaka 2017.
gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mpya uitwao Happy Birthday kisha mpe sapoti yako kwa kuwashirikisha na wengine kwa kadri uwezavyo ili waweze kubarikiwa kupitia wimbo huu. Karibu!
DOWNLOAD
0 maoni:
Post a Comment