Rapper wa Marekani mwenye asili ya nchini Morocco, French Montana amesikitishwa na kitendo cha ubaguzi kilichofanywa na shirika la ndege la Delta Airline kwa kumshusha abiria wake kwenye ndege hiyo kwa sababu ya kuongea Kiarabu.
Wiki hii kimeenea kipande cha video kinachomuonyesha kijana aliyefahamika kama Adam Saleh na rafiki yake Slim wakishushwa kwenye ndege hiyo wakati wakitaka kusafiri kuelekea mjini New York, Marekani.
“Guys, We’re getting kicked out because we spoke a different language. This is 2016. Delta airlines are kicking us out because we spoke a different language,” amesema Adam kwenye kipande hicho cha video.
Tukio hilo limeonekana kumgusa zaidi French baada ya kuamua kupost kipande hicho kwenye mtandao wa Instagram na kuandika:
“I don’t like speaking on things like this but this struck a nerve. I have a mother that doesn’t speak English and discrimination like this makes me really sad. The fact that this can happen to her makes me sick. I’m NOT using delta anymore smh #equality.”
0 maoni:
Post a Comment