Ivo Mapunda
Mlinda mlango wa zamani nchini Tanzania Ivo Mapunda amesema, hana mpango wa kuendelea kuvitumikia vilabu vya hapa nchini kutokana na viongozi wa vilabu hivyo kushindwa kuwathamini magolikipa ambao ni zao la hapa nchini.
Ivo
amewahi kuvidakia vilabu vya Tanzania Prisons, Moro United, Yanga SC,
St. George ya Ethiopia, African Lyon, Gor Mahia, Simba SC pamoja na timu
ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars".
Akizungumza na Hotmix Michezo Ivo amesema, vilabu vingi hapa nchini vimekuwa na fikra tofauti kwa magolikipa wa siku nyingi wa hapa nchini wakidhani wameshuka kiwango na hawawezi kutoa msaada wowote ndani ya timu suala linalomfanya yeye binafsi kushindwa kufanya kazi tena hapa nchini na kufikiria zaidi kucheza nje ya nchi.
Mapunda amesema, vilabu vingi hufikiria kuwa magolikipa wengi wanakuwa na mapenzi na klabu moja wapo hapa nchini hivyo kushindwa kumpa nafasi kwa kudhani hatocheza kwa faida ya timu bali atacheza kwa kuangalia timu anayoipenda zaidi.
Kwa upande wa vilabu vingi kuhitaji magolikipa kutoka nje ilihali hapa nchini kuna magolikipa wenye vipaji vizuri Ivo amesema, ni tatizo la uelewa wa viongozi wa vilabu kutokuwa na imani na wachezaji wa ndani wakiamini wengi wao hawana uwezo.
Mapunda amesema, mara nyingi vilabu hutafuta sifa kwa kutafuta magolikipa nje ya nchi na kupelekea magolikipa wazawa kukosa kabisa nafasi ya kuonyesha kipaji chao.

0 maoni:
Post a Comment