Mtanzania atwaa Tuzo ya Mjasiriamali Bora Afrika


















 Makamu Mwenyekiti wa TPSF Bw. Salum Shamte (kushoto) akimkabidhi kadi ya uanachama wa Taasisi hiyo Bi. Jennifer Shigholi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Dkt Godfrey Simbeye


Kijana wa Kitanzania, mwanadada Jennifer Shigoli ameshinda Tuzo ya Mjasiriamali Bora barani Afrika ijulikanayo kama African Entrepreneurship Award, na kutunukiwa zawadi ya dola za Marekani laki moja na nusu, zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 300

Bi. Jennifer ameibuka mshindi kutokana na kubuni mradi wa utengenezaji wa bidhaa za matumizi ya kike, mradi ulioonnesha kuwa na mchango mkubwa kwa jamii hasa kutokana na jinsi alivyoweza kutumia ubunifu wake kuzalisha ajira pamoja na suluhisho la mahitaji ya vifaa hivyo kwa wasichana wa vijijini.
Kutokana na ushindi huo, wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini chini ya Makamu Mwenyekiti wake Bw. Salum Shamte imeamua kumzawadia mwanadada huyo fursa ya moja kwa moja ya kuwa mwanachama wa TPSF, hasa kutokana na mtazamo alionao kijana huyo kuendana na dhana nzima ya TPSF ya kuhakikisha vijana wanakuwa chachu ya ustawi wa biashara unaoendana na mipango ya serikali ya kuwa taifa la uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment