Msanii wa rap Bongo Mwana FA amekiri kuwa ngoma ya rapa mwenzake Darassa, inayokwenda kwa jina la 'Muziki' imezipa wakati mgumu ngoma nyingine zilizotoka katika kipindi kimoja ikiwemo ngoma yake ya Dume Suruali.
Mwana FA (Kushoto), darassa (Kulia)

Mwana FA ametoa neno hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika kipindi cha FNL cha EATV na kutoa pongenzi nyingi kwa mkali huyo kwa kuzidi kuung'arisha muziki wa hip hop nchini Tanzania.
Mwana FA amesema kazi aliyofanya Darassa ni nzuri na inastahili kushika nafasi ya kwanza katika chati za muziki Bongo huku akiweka wazi kuwa ubora huo hauondoi ukweli kuwa yeye mwana FA ameanza muziki kabla ya Darassa na kwamba itakapofika Februari mwakani ngoma yake ya kwanza kuitoa itatimiza miaka 15.
"Kuhusu ngoma ya Darassa, ni kweli imezipa ngoma nyingine wakati mgumu ku-shine, lakini ikumbukwe kuwa ikifika mwezi wa pili mwakani, ngoma yangu ya kwanza itakuwa imefikisha miaka 15. Am Happy kwa muziki wa Rap, nafurahi kuona ngoma za rap zinatoka na zinakuwa hit, zinapiga bao nyimbo nyingine za kuimba"

Darassa
Pia amesema kilichombeba Darassa hadi kufikia hapa ni kutokata tamaa kama ambavyo aliimba kwenye ngoma yake iliyomtambusha ya 'Sikati Tamaa' miaka kadhaa iliyopita jambo ambalo wasanii wote wachanga wanapaswa kujifunza
"I'm happy for Darassa, namjua Darassa kwa muda mrefu, amekuwepo kwenye game kwa muda mrefu, mi namjua, anastahili kuwa namba moja sasa" Alisema Mwana FA