Polisi wa Ujerumani wamtambua muuaji wa watu 20 mjini Berlin


 

Polisi wa mjini Berlin wamefanikiwa kumtambua mtu aliyehusika kwenye shambulio la lori katika soko la Christmas, Berlin ambapo watu 20 walifariki dunia.
Anis Amri anayetuhumiwa kwa mauaji ya watu 20 mjini Berlin
Mtu aliyetambulika kufanya shambulio hilo ni Anis Amri (24) raia wa Tunisia ambaye ametajwa kuwa ni mmoja kati ya watu hatari ambaye amehusika kwenye mashambulio kadhaa.

Imedaiwa kuwa kijana huyo hutumia majina sita tofauti huku akiwa na uraia wa nchi tatu tofauti huku akidaiwa kuingia nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza mwaka jana.

Hata hivyo msemaji wa polisi wa mji wa Berlin amesema kuwa watahakikisha wanafanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo huku wakiahidi kutoa zawadi ya kiasi cha Euro 100,000 kwa mtu atakasaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment