WAFANYABIASHARA wa bidhaa za vyakula na vipodozi katika miji ya Mafinga na wilayani Mufindi mkoani Iringa na Makambako mkoani Njombe wamebainika kuwa vinara wa kuuza bidhaa zilizopita muda wake na kuhatarisha afya za walaji wao jambo ambalo limeelezwa kuwa wanalifanya kwa makusudi ili kujipatia faida pasipo kufikiri madhara kwa walaji.
Hayo yalibainishwa na mkaguzi kutoka mamlaka ya chakula na dawa TFDA mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini Yusto Wallace Alipokuwa akiteketeza bidhaa na vyakula vilivyopita muda wake na vile visivyokuwa na sifa za kuliwa na binadamu kutokana na kuwa na kiasai kikubwa cha sumu wakiwemo kuku wa kisasa ambao walikamatwa katika mji wa makambako.
Wallace alisema katika mji wa mafinga timu ya maafisa wa ukaguzi ilikamata zaidi ya tani 4 za bidhaa feki zenye thamani ya shilingi 3,500,000 na kuziteketeza mjini makmbako zoezi ambali lilienda sambamba na ukaguzi wa mji wa Makambako walikobaini uwepo wa vyakula feki vyenye thamani ya shilingi 8,300,000.
Aliongeza kuwa ukaguzi huo ni endelevu katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya nyanda za juu kusini na kwamba elimu zaidi inaendelea kutolewa kwa jamii ili kutambua bidhaa zisizo faa zinazoendelea kuuzwa.
Aidha alisema kumekuwa na tabia za wafanyabiashara kubadli alama zinazoonyesha bidhaa zilipitwa na wakati (expire date) na kuandika zinazonyesha muda ujao tatizo ambalo limejitokeza katika maeneo mengi.
”Kuna wanyabiashara hapa makambako tumekuta wanajaribu kuchezea muda wa matumizi kwa kufuta tarehe za kuisha muda wa matumizi wamekuwa wakibandika stika zinazoonyesha muda mrefu wa matumizi ingawa hatujajua mchezo huu unafnywa na nani kati ya wafanyabiashara na wasambazaji.” Wallace
Alieleza madhara makubwa yanayotokana na matumizi ya bidhaa zilizopita muda wake ni pamoja na kusanbaisha saratani ya ngozi au kuathiri mifumo ya uzazi kama kuharibika kwa mimba kwa akina mama wajawazito.
from Blogger http://ift.tt/2i2RwZF
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment