Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema, mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu anaifahamu Zanaco kuwa ni timu nzuri ambayo iliwahi kuiondosha Yanga mashindanoni wakati huo yeye ndio alikuwa anaingia kwenye kikosi hicho cha Jangwani.
“Zanaco ni timu kubwa, kipindi naingia Yanga tulishawahi kucheza nao, ni timu nzuri na ngumu na wamewahi kututoa kwenye mashindano. Naamini walimu watafanya kazi yao ili tuweze kufanya vizuri zaidi,” anasema nahodha wa Yanga ambaye alikaa benchi kwenye mchezo wa marudiano kati ya Yanga dhidi ya N’gaya.

0 maoni:
Post a Comment