Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa akiteta jambo na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete
Game ya Simba na Yanga ilifanya tofauti za vyama vya kisiasa
kukaa pembeni pale wanasiasa wa vyama viwili pinzani zaidi Tanzania
walipokutana kwenye jukwaa moja kushuhudia mechi hiyo kwenye uwanja wa
taifa. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Edward LowasaBila kutarajia, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Edward Lowasa
ambaye aligombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA alitinga
uwanjani na kukutana na wanasiasa mbalimbali wa CCM ambacho ni chama
alichokihama mwaka 2015 baada ya kukitumikia kwa muda mrefu. Mwenyekiti wa CHADEMA Freman Mbowe akisalimia mashabiki uwanja wa taifaLowasa aliambatana na mwenyekiti wa CHADEMA Freman Mbowe ambapo
walikutana na wenzao na wapinzani wao wa kisiasa kutoka CCM kama vile
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye Dar Derby. Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa ambaye aligombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA akisaliwa mashabiki wa sokaKitu kikubwa hapa ni namna soka lilivyo wakutanisha wanasiasa hawa
mashuhuri Tanzania na namna amani ilivyotawala huku wapinzani hao
wakubwa wakiwa Bungeni wakikumbatiana wakati wanasalimiana na baadae
kubadilishana mawazo wakiwa kwenye jukwaa moja. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akisalimiana na Simon Msuva wakati akikagua timu
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment