Msanii wa muziki wa hip hop,Nay wa Mitego amewakata kiu mashabiki wa muziki wake wa jiji la Dar es salaam kupitia show yake ya ‘Wapo Tour’ iliyofanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam.


Nay wa Mitego
Kabla ya show hiyo kuanza mvua kubwa ilinyesha na kusababisha baadhi ya mashabiki kusita kuingia lakini baada ya nusu saa mvua hiyo ilikatika na mashabiki kuigia kwa wingi.

Mashabiki wakicheza bila kujali mvua
Akiongea na Bongo5 muda mchache baada ya kumalizika kwa show hiyo, Nay aliwashukuru mashabiki wake kwa kujitokeza kwa wingi licha ya mvua kubwa kunyesha mapema kabla ya show kuanza.
“Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kujitokeza kwa wingi na kunionyesha upendo wao wa dhati. Mvua imenyesha kubwa lakini mashabiki walibaki kwaajili ya kuangalia show yangu hicho ni kitu kikubwa sana,” alisema Nay.

Barnaba

Wakali Wao wakifanya yao

Barnaba na Shilole

Barnaba na Shishi Baby

Nay na mashabiki wake

















0 maoni:
Post a Comment