KATIBA MPYA: Bunge kutuma ofisa Saudia kusimamia kura

Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. 
Ofisi ya Bunge la Katiba itamtuma ofisa wake kwenda Makka, Saudi Arabia kusimamia upigaji kura kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa wajumbe wa Bunge hilo wanaokwenda Hijja.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alipotakiwa kueleza idadi kamili ya wajumbe wa Bunge hilo wanaotarajiwa kuwa nje ya nchi na jinsi watakavyopiga kura.
Juzi, Bunge hilo lilizifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwaruhusu wajumbe watakaokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo wanaokwenda Hijja kuipigia kura Katiba inayopendekezwa, iliyokabidhiwa kwa Kamati ya Uongozi jana.
Chini ya marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya Bunge, ataruhusiwa kupiga kura ya wazi au ya siri kwa njia ya fax au mtandao kama itakavyoelekezwa na katibu kwa kushauriana na mwenyekiti.
Hamad alisema hadi kufikia jana mchana walikuwa wamewatambua wajumbe wanane ambao watakwenda Hijja huko Uarabuni lakini orodha ya watakaokuwa nchi nyingine bado haijajulikana.
Hamadi alisema ofisa wake huyo atasimamia kura za wajumbe wanaokwenda Hijja katika upigaji kura unaotarajiwa kuanza Septemba 29 hadi Oktoba 2 mwaka huu.

Wazanzibari 500,000 kupata vitambulisho


Na Rahma Suleiman

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imeanza kutoa vitambulisho vya taifa kwa wananchi  wa Zanzibar ambapo zaidi ya vitambulisho 500,000 vinatarajiwa kutolewa.

Mkurugenzi wa Nida Zanzibar, Vuai  Mussa Suleiman, alisema katika zoezi hilo wamejipanga vizuri ili kudhibiti maafa yasitokee kama yaliotokea wakati wa uandikishwaji wa zoezi hilo lililosababisha kifo na majeruhi.

Alisema kwa hatua za awali ugawaji huo umeanzia Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuwataka  wananchi wanapokwenda kuchukuwa vitambulisho vyao katika vituo walivyopangiwa wachukue stakabadhi  au vielelezo walivyopewa wakati wa uandikishwaji.

Alisema kama stakabadhi zao zimepotea, wanatakiwa kuchukua vitambulisho vingine ambavyo walivitumia wakati wa kujiandikisha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment