NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amekataa kuwalaumu washambuliaji wa timu yake kwa kutofunga mabao zaidi katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana.
“Tunamhsukuru Mungu tumeshinda, jambo muhimu hapa ni pointi tatu katika mchezo wa kwanza. Ligi Kuu ni ngumu kila timu imejiandaa, na mimi huwa sina kawaida ya kudharau timu,”amesema Cannavaro.
Beki huyo wa kati aliyetua Yanga SC mwaka 2006 akitokea Tembo ya Zanzibar, amesema kwamba mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa jana watayafanyia kazi ili wasiyarudie Jumatano dhidi ya Prisons.
Nahodha Cannavaro amesema ushindi muhimu kwa ajili ya pointi tatu, mabao mengi si hoja |
Mabingwa watetezi, Yanga SC jana wameanza vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na matokeo hayo kuipeleka Yanga SC kileleni mwa LIgi Kuu baada ya mechi nane za mzunguko wa kwanza, ikiongoza kwa wastani wa mabao, lakini ingeweza kuibuka na ushindi mnene zaidi kama washambuliaji wake wangetumia nafasi zaidi.
Mchezaji bora na mfungaji bora wa LigiKuu msimu uliopita, Simon Happygod Msuva alifunga bao la kwanza la Yanga SC msimu huu, dakika ya saba akimalizia pasi ya Amisi Tambwe, lakini akakosa mengine mawili ya wazi.
Mzimbabwe Donald Ngoma alifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 42 akimalzia mpira uliodondoka baada ya kugongwa kwa kichwa na beki wa Coastal, Tumba Lui Swedi aliyeruka na Mrundi Amisi Tambwe kugombea krosi ya Simon Msuva, lakini akakosa moja la wazi kipindi cha pili
Tambwe naye alikosa bao moja la wazi sawa na mawinga Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke aliyeingia kipindi cha pili.
from Blogger http://ift.tt/1Y6BwmS
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment