Arsenal hawana tatizo la katika safu yake ya ushambuliaji, hayo ni maneno ya Arsene Wenger ambaye pia anasema uwepo wa Alexis Sanchez, Olivier Giroud na Theo Walcott, unaweza kumpa magoli zaidi ya 20 kwa msimu.
Arsenal walihusishwa na usajili wa Karim Benzema na Edinson Cavani, lakini hata hivyo mambo yalikwenda ndivyo sivyo na badala yake kuamua kutonunua mshambuliaji yeyote.
“Nadhani Giroud, Walcott na Sanchez wanaweza kuleta magoli zaidi ya 20 bila tatizo lolote lile”, aliwaambia waandishi.
“Wakati mwingine lazima uwaamini wachezaji wako na kuwapa nafasi. Halafu baada ya muda watafanya vyema tu. Mara nyingi watu hutaka mafanikio ya haraka, lakini hatuendi hivyo.
“Nina Aaron Ramsey ambaye anaweza kufunga magoli 15, Mesut Ozil 15, Santi Cazorla 10. Vinginevyo, kama una mchezaji mmoja ambaye ndiye unategemea kwa ufungaji, siku akipata majeraha je?, nani atafunga sasa”.
Wenger amekosolewa kwa kutosajili mshambuliaji mpya katika dirsha la usajili lililofungwa mapema mwezi huu, lakini alilisisitiza kuwa kwa sasa washambuliaji hawapatikani tena katika bara la Ulaya.
“Washambuliaji wengi wanapatika nara la Amerika ya Kusini kwa sasa. Bara la Ulaya hawazalishi washambuliaji siku kabisa.
“Angalia nchi kama Ujerumani, ambayo ilicheza dhidi ya Scotland au dhidi ya Poland huku Mario Gotze ndio akiwa mshambuliaji wa mwisho – huyu ni kiungo. Si kana kwamba hawataki kumchezesha mshambuliaji halisi pale mbele lakini hayupo mshambuliaji ambaye ana vigezo vya kusimama pale mbele.
“Nani ambaye unamuona hapa Ulaya?”
“Kitu ninachoweza kusema ni kwamba, katika hizi akademi za soka zinatakiwa kuwatenegeneza washambuliaji tangu wakiwa katika umri mdogo. Kuna umri kati ya miaka mitano mpaka 12 ambapo ndipo unaweza kutengeneza kipaji cha maana. Umri katika ya miaka 12-14 unaanza kumtengeza katika kasi yake na nguvu katika mwili.
from Blogger http://ift.tt/1K9sCgU
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment