Kocha wa Manchester United Louis van Gaal, amekiri kwamba humuwia vigumu sana kuelewa pindi anapozungumza na nahodha wake Wayne Rooney .
Van Gaal amemsifu Rooney na kusema kuwa ni moja ya wachezaji watano bora ambao amewahi kuwafundisha katika maisha yake ya soka.
Alipoulizwa kuhusu kuelewana vyema na Rooney, Van Gaal alijibu, lafudhi ya Rooney humpa wakati mgumu sana pindi wanapowasiliana.
“Wakati nikiongea, huwa natamka maneno vizuri tu”, Van Gaal aliiambia RTL4’s ‘Linda’s Zomerweek’.
“Kama ukimuweka Wayne Rooney katika siti hii, na ukaanza kuzungumza naye, unadhani kuwa watu watamuelewa Wayne Rooney? huwezi kumuelewa kamwe anachokizungumza”.
By bkmtata.com
from Blogger http://ift.tt/1K9sEWb
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment