Viongozi wa Kenya waishambulia korti ya ICC


Viongozi wa Kenya waishambulia korti ya ICC
Viongozi mbalimbali nchini Kenya wakiwemo wabunge na maseneta wameishambulia vikali Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wakisema korti hiyo inalenga kuiaibisha nchi yao kimataifa. 
Viongozi na wanasiasa wametoa kauli hiyo baada ya ICC kutoa waranti wa kukamatwa wakili mmoja na mwanabiashara mmoja; wote wawili wakiwa ni raia wa Kenya. 
ICC inadai kwamba, wawili hao wamekuwa wakijaribu kuvuruga kesi za Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na mwandishi wa habari, Joshua Sang. Wakili Paul Gicheru na mwanabiashara Philip Kipkoech wanadaiwa kuwashawishi mashahidi kuondoa ushahidi wao dhidi ya Ruto na Sang. 
Kiongozi wa shughuli za serikali katika bunge la Seneti, Dk. Kithure Kindiki amesema ICC imepoteza itibari na kwamba hali ikiendelea hivyo, Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliopelekea kuundwa korti hiyo ya kimataifa.

from Blogger http://ift.tt/1XZQ33w
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment