Bunge la EU laridhia kusitisha kwa muda mazungumzo ya uanachama wa Uturuki


Mvutano wa Uturuki na Ulaya waongezeka

Bunge la EU laridhia kusitisha kwa muda mazungumzo ya uanachama wa Uturuki

Bunge la EU limepiga kura na kukubaliana kuutaka Umoja huo kusimamisha mazungumzo kuhusu ombi la Uturuki kutaka kuwa mwanachama wa EU
Bunge la Ulaya limeidhinisha kwa sauti kubwa ya kura 479 dhidi ya kura 37 kuzuia yasiendelee mazungumzo yanayohusu ombi la Uturuki kujiunga na  Umoja wa Ulaya.Wabunge 107 walijizuia kulipigia kura azimio hilo ambalo hata hivyo halizifungi kisheria nchi za Umoja huo.Azimio hilo kimsingi linataka mazungumzo hayo yasimamishwe hadi pale serikali ya mjini Ankara  itakapoziondoa hatua zake zinazovuka mipaka chini ya sheria ya hali ya dharura.
Licha ya hatua hiyo ya bunge la Umoja wa Ulaya maafisa wa Umoja huo wamesema kwamba mazungumzo hayo yaliyochukuwa muda mrefu bila ya kupata mafanikio hayapaswi kusimamishwa mara moja.Baadhi ya nchi za Umoja huo wa Ulaya zimetowa mwito wa kufutwa kabisa kwa mazungumzo hayo lakini taasisi hiyo inafanya juhudi ya kufikia msimamo wa pamoja ambao utaleta uwiano katika kile inachokitaka nchi wanachama wake kwa Uturuki ambacho ni kuendelea kusaidia kuzuia mamia kwa maelfu ya wakimbizi wanaoelekea ulaya pamoja na kushughulikia wasiwasi wa nchi hizo kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu.
Türkei Omer Celik (picture alliance/abaca/E. Aydin) Omer Cemik-Waziri wa Uturuki anayehusika na mazungumzo ya kujiunga EU
Kiongozi wakundi la waliberali la ALDE katika bunge hilo Guy Verhofstadt amesema kwa kuendeleza njozi ya kuwa na mazungumzo ya tija kuhusu uanachama wa Uturuki,nchi ambayo inazidi kila kukicha kuimarisha utawala wa kiimla,Umoja wa Ulaya utapoteza kabisa hadhi yake nauaminifu wake na pia utakuwa unawapotosha raia wake sambamba na kuwahujumu raia wa Uturuki wanaooutegemea Umoja huu wa Ulaya katika hatma ya nchi yao.
Ingawa hatua hiyo ya bunge haina athari za haraka za moja kwa moja lakini inaonesha ni kwa jinsi gani Umoja huo wa Ulaya unazidi kukerwa na hatua za rais Reccep Tayyip Erdogan  za kuimarisha mipango ya kubakia madarakani  kupitia  jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa.
Türkei Rede Erdogan bei der Sitzung der Parlamentarischen Versammlung der NATO in Istanbul (Reuters/M. Sezer) Rais wa Uturuki-Reccep Tayyip Erdogan
Erdogan binafsi ameshasema kwamba hatua ya bunge la Umoja wa Ulaya haiwezi kuyumbisha juhudi za kuimarisha usalama na mustakabali wa nchi yake. Maelfu ya watu wakiwemo walimu,waandishi habari na wabunge wa upinzani wamekamatwa au kufutwa kazi huku ripoti zikisema kwamba watu zaidi wataendelea kukamatwa na kukandamizwa.Mjini Ankara kwenyewe waziri anayehusika na jukumu la kusimamia mazungumzo hayo pamoja na nchi za Ulaya Omer Celik amezikosoa nchi za Umoja huo kwa kushindwa kusimama pamoja na serikali ya Uturuki katika wakati ambapo inakabiliana na wimbi la Mashambulizi.
Leo (24.11.2016)Ofisi ya waziri mkuu imezuia kwa muda harakati za kuripoti juu ya shambulio la bomu  lililotokea  asubuhi katika mkoa wa Adana kusini mwa Uturuki ambapo watu wawili wameuwawa na zaidi ya 16 wamejeruhiwa.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment