Mji wa kale wa zaidi ya miaka 5,000 wagunduliwa Misri



Mji wa kale wa zaidi ya miaka 5,000 wagunduliwa Misri

  • Saa 9 zilizopita
Image copyright Egyptian Ministry of Antiquities
Image caption Mji huo huenda ulikuwa makao ya wachimbaji na wajenzi wa makaburi
Wanaakiolojia nchini Misri wamegundua kile wanachosema ni mabaki ya mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 5,000 iliyopita.
Wamepata nyumba, vifaa, vyungu na makaburi makubwa.
Mabaki hayo yamo eneo la ukingo wa mto Nile, karibu na hekalu la Seti, eneo la Abydos.
Wataalamu wanasema makaburi 15 yaliyogunduliwa yanaashiria kwamba ni watu wa hadhi ya juu waliozikwa humo.
Inaaminika kwamba mji huo ulikuwa makao ya maafisa wakuu wa serikali na wachimbaji na wajenzi wa makaburi, ambao ulifana enzi za kwanza kabisa za Misri ya kale.
Wataalamu wanasema ugunduzi huo huenda ukasaidia kufufua sekta ya utalii nchini humo ambayo imeathirika pakubwa kutokana na machafuko yaliyofuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.
Image copyright Egyptian Ministry of Antiquities
Image caption Picha inaonesha kile ambacho wataalamu hao wanasema ni makaburi yaliyogunduliwa katika mji huo
Wanaakiolojia wanasema wamegundua vitu vingi kwenye mji huo vikiwemo majumba, vigae vya vyungu na vifaa vilivyoundwa kwa kutumia chuma na mawe.
Lakini mtathmini wa BBC wa masuala ya Mashariki ya Kati Alan Johnston anasema muhimu zaidi ni makaburi yaliyogunduliwa.
Inaaminika kwamba maafisa wakuu na wajenzi wa makaburi, ambao huenda walihusika katika kujenga makaburi ya kifalme katika mji mtakatifu wa Abydos hapo karibu waliishi eneo hilo. Mji wa ABydos una mahekalu, na unaaminika kutumiwa kama mji makuu wakati mmoja enzi za kale za utawala wa Misri.
Image copyright Egyptian Ministry of Antiquities
Image caption Baadhi ya vitu vilivyogunduliwa eneo ambalo wataalamu wanasema kulikuwa an mji zaidi ya miaka 5,000
Image copyright Getty Images
Image caption Maeneo ya akiolojia karibu na Luxor (pichani) na kwingineko Misri yametatizika kuwavutia watalii kutokana na misukosuko ya kisiasa


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment