Renminbi itaimarika katika mfumo wa fedha duniani

Renminbi itaimarika katika mfumo wa fedha duniani


Naibu mkurugenzi wa Benki Kuu ya China Bw. Yi Gang jana amesema, Renminbi itaendelea kuimarika katika mfumo wa fedha duniani.

Hivi karibuni, kiwango cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi za China kwa dola za Marekani kimepungua kwa asilimia 3.5 tangu mwezi Oktoba. Bw. Yi Gang amesema, kuongezeka kwa thamani ya dola za Marekani kunasababishwa na hali mbalimbali nchini humo, kama vile kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini Marekani, matarajio ya mfumuko wa bei na uwezekano wa kuongeza riba ya Benki Kuu ya Marekani. Kiwango cha ubadilishaji wa Renminbi ya China kwa dola za Kimarekani sio kubwa ikilinganishwa na kiwango cha ubadilishaji wa fedha nyingine dhidi ya dola za Marekani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment