‘Kamusoko aliimaliza Yanga’ – Shaffih Dauda



Mchambuzi wa masuala ya michezo kutoka Clouds Media Group Shaffih Dauda amesema, kiungo wa Yanga mzimbabwe Thaban Kamusoko ndiye aliyeiua Yanga kwenye mchezo wao dhidi ya Simba jana Jumamosi February 25, 2017.

Dauda amesema, kuumia kwa Kamusoko na kushindwa kuendelea na mchezo lilikuwa ni pigo kwa Yanga huku Simba wakitumia mwanya huo kutawala zaidi eneo la katikati ya uwanja na kutekeleza mipango yao ya mashambulizi golini kwa Yanga.

“Kamusoko ni mchezaji wa kimataifa, miongoni mwa wachezaji wan je wenye viwango vya juu kwenye ligi ya Tanzania tangu alipojiunga na Yanga akitokea FC Platinum ya nyumbani kwao Zimbabwe,” alisema Shaffih wakati wa uchambuzi wake kwenye kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FC.

“Anauzoefu mkubwa na mechi za kimataifa na mechi kubwa kama ya Simba na Yanga, ameshacheza mechi zote za Simba na Yanga tangu asajiliwe na Yanga. Wakati yupo uwanjani alikuwa akishirikiana vizuri na Zulu kutibua mipango ya Simba kuelekea kwenye eneo la ulinzi la Yanga hivyo kuwafanya mabeki wa Yanga kuwa salama muda mwingi kipindi cha kwanza.”
“Baada ya kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na majeraha aliyoyapata, benchi la ufundi likalazimika kufanya mabadiliko yasiyo ya kiufundi kwa kumwingiza Said Juma Makapu kuzipa nafasi ya Kamusoko.”

“Makapu alishindwa kufikia uwezo uliokuwa ukioneshwa na Kamusoko, ambaye alikuwa alikuwa akisaidia ulinzi na kuipandisha timu wakati inashambulia.”

“Badae dakika ya 78 wakati Simba ikiwa imeshasawazisha goli, Lwandamina akamwita nje Justine Zulu na kumwingiza Juma Mahadhi kwa lengo la kushambulia zaidi ili kupata goli jingine, lakini kwenye safu ya kiungo wa ulinzi akabaki Makapu peke yake mwisho wa siku akazidiwa na Said Ndemla na Mkude sambamba na Ajibu ambaye alikuwa anashuka chini kuchukua mipira na kupelekea Simba kupata bao la pili.”

Kamusoko aliumia mkuu wa kulia na kupatiwa matibabu na madaktari wa Yanga, aliendelea kidogo lakini badae alishindwa kuendelea na akalazimika kutoka kwa msaada wa machela.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment