Mwamuzi Mark Clattenburg anunuliwa huko Saudi Arabia

KWELI siku zinakwenda kasi sasa. Siku hizi hadi waamuzi wa soka wananunuliwa kama ilivyo kwa
wachezaji.
Hivi karibuni hilo limetokea kwa mwamuzi mashuhuri Ligi Kuu England, Mark Clattenburg. Image result for Mark Clattenburg
Imefichua kwamba Clattenburg aligomea ofa ya Pauni 1 milioni kutoka China kabla ya kuamua kuachana na Ligi Kuu England na kuhamia Saudi Arabia.
 Clattenburg (41), sasa atakuwa anavuna Pauni 500,000 kwa mwaka ambazo hazikatwi kodi kwa kuwa mkuu wa waamuzi katika Shirikisho la Soka la Saudi Arabia. 
Kiwango hicho cha pesa ni
mara mbili ya kile alichokuwa akivuna.
Mwamuzi mwingine wa zamani wa England, Mark Halsey amesema si suala la pesa bali uongozi mbaya wa marefa ndio uliomfanya Clattenburg aamue kuachana na Ligi Kuu England na
kutimkia
Clattenburg ni mwamuzi maarufu sana kwenye Ligi Kuu England na kuondoka kwake kunatajwa kuwa ni pigo kwenye soka la nchi hiyo,
 hasa ukizingatia alikuwa kioo cha waamuzi
wanaochipukia.
Clattenburg alichezesha mechi ya fainali ya Euro na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana na kwamba amejichora tattoo kwa ajili ya kumbukumbu ya mechi hizo kubwa kabisa kwake.
Ndoto zake za kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia ilishindwa kutimia baada ya Mwingereza mwenzake Howard Webb na Mtaliano Nicola Rizzoli kuchezesha fainali mbili
zilizopita za karibuni za kombe hilo. 
Kwa uamuzi huo wa Clattenburg ina maana kwamba mechi yake ya mwisho kuchezesha England ni ile ya Arsenal na Hull City, ambapo vijana wa Wenger walishinda 2­0.
Moja ya matukio yenye utata yanayomhusu mwamuzi huyo ni tukio lile la mwaka 2012 lililodaiwa Clettenburg alitumia lugha za kibaguzi dhidi ya Juan Mata na Mikel Obi kipindi hicho
walipokuwa klabuni Chelsea.
Hata hivyo, chama cha soka cha England kilimsafisha kwa kashfa na kudai kwamba hakutenda kitendo hicho cha kuwabagua wakali hao wa Stamford Bridge kwa kipindi hicho. 

from Blogger http://ift.tt/2m8kINL
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment