RIDHIWANI KIKWETE KURITHI MIKOBA YA KINANA CCM

Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa hajawahi kutamani Urais wa Tanzania bali anatamani siku moja awe Katibu Mkuu wa CCM ambayo kwa sasa inashikiliwa na Abdulrahman Kinana. Alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano aliyofanya na kipindi kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Clouds, Clouds 360.
Ridhiwani aliulizwa endapo ana ndoto za kuwa Rais wa nchi hii ambapo alijibu kuwa, “Sijawahi kutamani kuwa Rais ila muda ukifika natamani kuwa Katibu Mkuu wa CCM,” alisema.
Ridhiwani alisema kuwa mafanikio yake hadi hapo alipofikia ni kutokana na mchango wa baba yake ambaye ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete. “Malezi yangu, kuzaliwa na kiongozi kumenisaidia kufikia hapa, nisingezaliwa huko labda ningekuwa mtu tofauti na nilivyo. Mzee wangu ana mchango mkubwa hata jimboni, ananipa changamoto, ananielekeza, ana nafasi ya kunishauri,” alisema.
Pia, alisema katika kutekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda, tayari mkoa wa Pwani una viwanda 164 vikiwamo vinavyojengwa na vilivyokamilika, huku 84 vikiwa ni vikubwa. Alisema uwekezaji wa viwanda hivyo umegawanyika katika sehemu mbili, chini ya shilingi bilioni tano na ule ulio juu zaidi. “Sehemu kubwa ni viwanda vya kuchakata malighafi, kuna vya matunda, marumaru, nondo, korosho, mabati, saruji na malighafi ya nyumba na vinavyofanya kazi nikivitaja ni zaidi ya 40,” alisema.
ANGALIA VIDEO CHIDEO

from Blogger http://ift.tt/2mrZ5ZB
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment