Kampuni ya Magari
ya Uber, ya Marekani, imekiri kutumia programu ya kisiri ya kompyuta,
kuisaidi kutambua na kuwazuia wakaguzi kupata taarifa,inayotoa ushahidi
wowote kwamba inavunja sheria inayoongoza huduma ya usafiri wa texi.
Programu
hiyo imeundwa kwa njia ya kipekee, kuwakinga madereva wa kampuni hiyo,
dhidi ya watumizi ambao wanaweza kuwawekea mtego kwa lengo la
kuwakamata.Gazeti la The New York Times imefichua kuwa kampuni ya Uber imetumia programu hiyo ya kisiri kuendesha shughuli zake katika miji kama vile Boston na Paris, Hali kadhalika katika mataifa ya Australia, Italia,na China.
Kampuni ya Uber inakabiliwa na tuhuma za ubaguzi kwa misingi ya kijinsia , ushindani mbaya, unaotokana na mtindo wake wa usimamizi na vile vile kuwapunja madereva.
0 maoni:
Post a Comment