Basi lililogonga mti nchini ZimbabweHerald
Watu 43 wamepoteza maisha nchini Zimbabwe baada ya basi la abiria walilokuwa wanasafiria kukosa mwelekeo na kugonga mti.
Msemaji
wa Polisi Charity Charamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika
eneo la Nyamakate karibu na nchi ya Zambia siku ya Alhamisi.
Wafanyibiashara mara nyingi hutumia usafiri wa mabasi kati ya nchi hizo mbili kusafirisha bidhaa na kufanya safari nyingine.
Mwaka uliopita, watu 30 walipoteza maisha wakati abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Jijini Harare na Bulawayo kupata ajali.
Watalaam wanasema kuwa ajali nyingi zimeongezeka katika nchi ya Zimbabwe na nchi zingine za Kusini mwa Afrika kutokana na ubovu wa barabara.

0 maoni:
Post a Comment