Mtu
mmoja aliyefahamika kwa majina ya Lughano John aliye na miaka 36 mkazi
wa Ipinda Juu ameuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na
wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia sheria mkononi baada
ya marehemu kutuhumiwa kuwa ameiba baiskeli.
Tukio
hilo limetokea jana asubuhi ya saa nne katika kitongoji chaLutusyo,
kijijini Talatala katika Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani hapa
Mbeya.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio zinaeleza kwamba
marehemu Lughano John alikamatwa na wananchi hao akiwa na baiskeliya wizi na kisha kuanza kumshambulia kwa kumpiga hali iliyopelekea kifo chake.Wakati msako wa kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo ukiendelea, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitishia Fichuo Tz kutokea kwa tikio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawe na tabia ya kuwapeleka watuhumiwa wanaokwamatwa katika mamlaka husika.

About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni:
Post a Comment