Balozi Seif akemea chokochoko za kidini


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amesema viongozi wa kidini wanapaswa kuwa macho kuzikataa choko choko na ushawishi unaotolewa na wanasiasa.

Alisema kazi inayotakiwa kufanywa na viongozi hao ni kuwaombea watu wakiwemo viongozi wa nchi ili baraka ziongezeke ndani ya taifa pamoja na umma jambo ambalo litasaidia kupunguza misuguano.

Alisema hayo wakati akilifungua tamasha la kuliombea taifa na kuhamasisha amani, linalofanyika ukumbi wa Masai Laugwa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema amani na utulivu wanaojivunia Watanzania miaka mingi sasa ni miongoni mwa neema zinazopaswa kutumiwa vizuri.

Alisisitiza njia nzuri ya kuzitumia neema hizo ni kwa wananchi kuzidisha juhudi katika uzalishaji mali wiwandani na mashambani, kuzidisha upendo na mshikamano bila ya kujali rangi, kabila au asili ya mtu.

Aliitahadharisha jamii kutotoa nafasi kwa watu wenye nia mbaya ya kutaka kuliangamiza taifa na kulitumbukiza kwenye vurugu na mapigano.

“Mimi kamak wa serikali kwa kushirikiana na viongozi wenzangu na wananchi wenye nia njema na taifa letu tutaendelea kufanya kazi wakati wote na tutahakikisha amani na utulivu inadumu 
ndani ya nchi yetu ambayo ndio maisha yetu,” alisema.

Alitoa wito kwa akina mama kuendelea kuwa walinzi na 
wasimamizi wa amani na utulivu.

Alisema mara nyingi wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa wa vurugu, hivyo amani ndio suluhisho pekee la 
kuwalinda.

“Mara nyingi tunashuhudia kwenye vyombo vya habari jinsi wanawake na watoto wanavyokufa au kujeruhiwa kutokana na 
vita vinavyozuka katika maeneo yao,” alisema.

Akizungumzia dawa za kulevya ambazo ni tishio a vijana, alisema serikali inachukua juhudi kupambana na janga hilo.

Alisema serikali zote mbili zinachukua hatua za makusudi katika viwanja vya ndege na bandari kwa kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu na kupunguza kasi ya 
uingizaji.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment